GET /api/v0.1/hansard/entries/496723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 496723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/496723/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii kuweza kuchangia mjadala ulio mbele yetu. Ni huzuni kwa Wakenya wengi ambao wametoka hapa nchini kuelekea huko Saudi Arabia kutafuta malisho mema ilihali inageuka kuwa si malisho mema bali ni kifo. Hivi ninavyozungumza kuna msichana mmoja kutoka katika eneo Bunge langu kwa jina Santa Kassim. Yuko Lebanon na anadai kwamba anahitaji kurudi nyumbani na ameitishwa Kshs200,000 ndio aweze kurejeshwa nyumbani. Wazazi wake wamejaribu na wamepata Kshs50,000. Kilichosalia ni Mhe. Mbunge aongeze zilizosalia ili msichana huyo arudi nyumbani. Ni jambo la kusikitisha kwamba watoto wetu wanatoka hapa nchini wakienda huko Uarabuni tukiwa pia sisi wazazi tunafahamu kwamba Waarabu walitutesa kwa miaka mingi. Tukiwa ni watumwa na hivi sasa bado watoto wetu wanaenda kuwa watumwa wakupenda. Si kupenda vile ni kwasababu nchini, pia hali ya ajira imekuwa duni na hivyo basi inalazimu vijana wetu watoke nje. Mapendekezo yangu ni kwamba Serikali ya Kenya iweze kuchukua hatua na kuona kwamba Serikali ya Saudi Arabia inalipa ridhaa kwa jamii ambazo watu wake wamepoteza maisha wakiwa nchini Saudi Arabia. Vile vile, wale maagenti wanaojihusisha na biashara hii haramu wachukuliwe hatua inayofaa maana hawana tofauti na wale walanguzi wa dawa za kulevya. Biashara hii yakuuza binadamu kwa jina la kwamba wanaenda kazini ni jambo ambalo Serikali ya Kenya haistahili kamwe kuiruhusu kuendelea. Vile vile, ningependekeza kwamba afisa mhusika wa mambo ya nchi za kigeni, wakati hawa wanatoka, ingelazimu wasajiliwe sawasawa ili wapate kujulikana ni kina nani ambao wametoka hapa nchini kuenda kutafuta kazi nchi za nje. Tumepata pia matangazo kutoka kwa nchi ya Uingereza kwamba wanaweza kupata kazi au kusoma wakiendelea na kazi lakini hayo yote, mwisho hayatuletei matunda hapa nchini bali yanatuletea madhara mazito. Serikali ya Kenya inastahili kuchukua hatua mwafaka kuona kwamba inawaokoa watu wake. Kwa hayo, ningetaka kumpongeza pia Mheshimiwa aliyeleta Hoja hii. Asante."
}