GET /api/v0.1/hansard/entries/497035/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 497035,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497035/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nichangie mjadala huu. Kwanza, ningependa kuunga mkono kwa kusema kuwa maji ni uhai. Sote tunatumia maji kwa haja nyingi za kimaisha, kukiwemo kilimo na kadhalika. Katika Kipengee cha 43 cha Katiba yetu ya Kenya, tunaona kuwa maji ni haki ya kila mwananchi. Katika usimamizi wa sekta hii ya maji, ninaunga mkono kuwepo kwa bodi za usimamizi. Lakini, lazima zihuzishe washika ndau wote, hasa wananchi ambao hutumia bidhaa hii. Ukiangalia katika Kaunti ya Taita Taveta, maji yanapitia kwangu ndio yaende katika Kisiwa cha Mombasa. Lakini cha kushangaza ni kuwa sehemu za Mikindani, Miritini, Jomvu, Mikanjuni, Kasarani, Kizurini, Mugusi na nyingine nyingi, ambako maji haya yanapitia, mpaka sasa watu wanaishi katika hali ambayo hawawezi kupata bidhaa hii adimu; maji. Kwa hivyo, kuundwa kwa bodi hizi kutaweza kuhusisha washika dau wote ili kuona kuwa sehemu zote, ambako wananchi wanatakikana kutumia maji haya, wanayatumia ili waweze kupata haki yao ya kikatiba. Mswada huu ni lazima pia uzingatie zaidi mbinu za kuchimba mabwawa ya maji katika sehemu nyingi ambazo hazijapata njia za kupata maji. Hii itawezesha kuona kuwa wakati ambapo hakuna mvua, wale ambao wameweza kuvuna maji katika mabwawa wataweza kuyatumia kwa kilimo na vile vile matumizi mengine maishani. Ninaunga mkono Mswada huu. Vile vile, nikiangalia kauti yangu ya Mombasa, ninampongeza gavana wangu; Ali Hassan Joho, kwa sababu maji ameyapa kipaumbele. Vile vile, ameona kuwa bali na kufanya juhudi katika kaunti, tunawavuta wafadhili kutoka nchi ya Ujerumani ili waweze pia kuwasaidia wananchi wetu wa Mombasa katika shida hii ya maji. Kwa hivyo, Mswada huu ukipitishwa, nina imani kuwa tutaweza kusaidia jamii katika sehemu zetu, hasa, katika sehemu yangu ya Jomvu, kwa jumla. Shukrani sana, Mhe Naibu Spika wa Muda."
}