GET /api/v0.1/hansard/entries/497371/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 497371,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497371/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ninasimama kuunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na rafiki yangu, Sen. Njoroge. Ninamshukuru Sen. Njoroge kwa fikra zake. Hii inaonyesha kwamba uteuzi aliopewa na chama kilichomteua kuja hapa,umeanza kuzaa matunda. Jambo linalozungumziwa hapa ni jambo muhimu sana. Linaanzia kwa kutambuliwa kama “walemavu”. Kwa wale ambao wanataka kutumia lugha ya madharau, wanawaita “wasiojiweza”. Halafu wale wenye matusi ya juu wanawaita “viwete”. Watu hawa ni viumbe vya Mungu na hatujui tutamuita mtu nini ambaye ana ugonjwa wa roho au mtu ambaye ana vidonda vya tumbo. Lakini sisi sote kama binadamu, kuna sehemu fulani katika miili yetu ambayo inatubidi tukumbuke Mungu wetu na kumwomba. Lakini hatuna majina kamili tunayoitwa ila tu hawa wengine. Bw. Spika wa Muda, tangu tunyakue Uhuru hapa nchini Kenya, watu ambao wana maumbile tofauti wamebaguliwa na hadi kufikia kiwango cha kujihisi kwamba hawastahili kuishi. Kuna mwimbaji mmoja kwa jina Daudi Kabaka ambaye aliimba wimbo akisema kwamba, ukizuru katika kila mji wa taifa letu la Kenya, katika barabara ya kila mtaa, utakuta mtu ambaye hajiwezi. Na kama ni mwanamke, utampata kwamba amepachikwa mimba. Daudi Kabaka anauliza: Je, mimba hii ni kutoka kwa mtu ambaye hajiwezi ama ni kutoka kwa yule anayejiweza na nia yake ni kumuumiza yule ambaye hajiwezi? Haifai wanaojiweza kuwatusi na kuwadharau wale ambao hawajiwezi, hasa wanawake. Baada ya kuwapachika mimba, huwa wanawatoroka. Katika taifa letu, wakati kazi za kijeshi zinapotangazwa, huwezi kuwapata watu hawa katika mstari wa mbele wakitafuta kazi katika jeshi, askari polisi au askari jela. Hawaajiiriwa katika kazi ambazo zinastahili mtu atumie nguvu zake. Lakini wao hulipa kodi hata wakiwa ni wa kuombaomba, kama mtu yeyote nchini. Akinunua sukari nusu kilo, analipia kodi. Lakini hata wakati tuna sherehe zetu za kitaifa, utashangaa kuona kwamba hao ndugu zetu, dada zetu na watoto wetu hawatengewi sehemu yao katika sherehe hizo. Iwe ni sherehe yoyote, sijaona hata kiti kimoja kilichotengewa watu hao. Kwa hivyo, watu hawa wamebaguliwa katika nchi yao. Bw. Spika wa Muda, ninamshukuru Sen. Njoroge kwa sababu Mswada huu ukipita itabidi watu hawa wahesabiwe upya ili tujue idadi yao. Ikiwa wamefika milioni kumi ama ishirini, kiwango chao katika mgao wa mapato wa hii nchi ya Kenya ni nini? Leo ninasema haya kwa sababu mpango tunaoendesha wa “Okoa Kenya”, tumesema kwamba baadhi ya mambo tunayotaka – ningependa wanasheria wayasikie haya – tunasema kwamba katika kazi za Serikali, yale “makabila makubwa” wasipate zaidi ya asilimia 15 ya kazi za nchi yetu. Lakini wale ambao ni chini ya asilimia 3, tunasema wapewe asilimia 30 ili wao pia wajivunie taifa lao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}