GET /api/v0.1/hansard/entries/497373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 497373,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497373/?format=api",
    "text_counter": 261,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Pia, ningependa wale wanaorekebisha sheria yetu wahakikishe ya kwamba watu hawa wanapate asilimia fulani katika mgao wa kazi za umma ili wasitengewe pesa ilhali hatujui idadi yao na hawajulikani wanakoishi na vile wanavyojikimu kimaisha halafu zile pesa zinaenda kwa mifuko ya watu binafsi ambao hawana ulemavu wowote. Hakuna hata mtu mmoja asiyejiweza atafaidika ili ajiweze. Pesa nyingi zimepeanwa katika kaunti zetu ilhali hakuna kaunti katika nchi hii yetu ambayo inaweza kuonyesha kwamba imesaidia watu hawa. Nilimsikia Sen. Mutula Kilonzo Jnr. akisema kwamba yeye amewahi kuwasaidia kwa kuwanunulia viti ambavyo wanatumia. Kila mwaka, ninatoa zaidi ya viti hamsini kwa hawa watu ambao Mungu amewaumba tofauti nasi. Hivi sasa, nimeitishwa viti 30 na Mhesimiwa Mwikali kutoka kaunti ya Busia, kaunti ya Kitui nimeitishwa 20 na kule Machakos nimeitishwa 10. Kwa hivyo, ninatarijiwa kuwa na viti 60."
}