GET /api/v0.1/hansard/entries/497377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 497377,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497377/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Anawabeba wapishi wake akienda Kitui. Pia anabeba kiti chake kwa sababu viti vingine vina chawa na hataki kubeba chawa. Anabeba mkeka mwekundu kama huu ili utandikwe akanyage. Haya yote yanafanyika katika kaunti ambayo watu hawajui wanaenda wapi. Ukiangalia miguu ya mtu huyu huwezi kusema kama anakula chakula. Fikiria juzi tuliona katika runinga mtu mmoja ambaye anaandika kutumia mguu wake, vidole vya miguu yake vinashika kalamu anapoandika. Huyo mtu anajifanyia kazi na hiyo miguu yake kuandakia lakini nchi ina Gavana, anatembea na magari 20. Nchi ambayo ina waziri ambao kila mmoja wao anapewa magari matano, walinzi 20 na nyumba zinalindwa. Mtu mmoja gharama yake kwa mwezi ni zaidi ya Ksh10 milioni na kuna mwingine ambaye hata viatu vya kutembelea hana. Mheshimiwa Spika wa Muda, namshukuru Seneta Njoroge kwa kuleta Mswada huu. Mungu atakubariki. Tutachangia Mswada huu na tujitole kuona kwamba wale ambao ni wa nyuma wanaenda mbele na wale ambao walikuwa wa mbele wana rudi nyuma kidogo. Haya ninaongea hata katika siasa. Nikiongea watu wengine wanafikiri kwamba ninamlenga mtu fulani. Taifa ni letu na haki zote ni zetu. Mungu aliumba nchi hii iwe yetu. Haijailishi wewe ni nani. Nataka kumwambia Seneta Njoroge aendelee na kazi hii nzuri amefany hapa na wapiga kura wetu watatambua mchango wake. Kama baiskeli hampti, hakuna mmoja wenu anaweza kuwa rais katika Kenya. Hii ndio sababu ninapendekeza tubadilishe upigaji wa kura ili uweze kupigiwa kura sio kwa sababu kabila yako ni kubwa, yangu ni ndogo au ya Seneta Hassan ni ya kati kati, unaweza kupata kura za kaunti 47 na kuwa rais wa taifa letu bila kubaguliwa unatoka wapi au walala wapi. Mambo haya yatafanya Mungu atubariki na tuunganishe taifa letu. Kama ingekuwa Mheshimiwa Moi ningesema alivyo kuwa akisema kwamba: “Na hapo ninafunga.”"
}