GET /api/v0.1/hansard/entries/497555/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 497555,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497555/?format=api",
"text_counter": 158,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza, nataka kumpongeza mhe. Chris Wamalwa kwa kuuleta huu Mswada na kidogo ni mlaumu kwa sababu amechelewa sana. Huu ni Mswada ambao ungeletwa Bungeni mwaka mmoja na nusu uliopita wakati tulipoingia Bungeni. Hii ni kwa sababu ni muhimu sana kuwatambua mashujaa wetu ambao wametuletea nafasi nzuri na faida katika nchi hii. Vile vile, ningetaka kumshukuru yule ambaye ameuleta Mswada kwamba kila kaunti iwe na chuo kikuu. Hili ni jambo la maana na ambalo litahakikisha kwamba elimu, ambayo ndiyo mwenge katika ulimwengu na maisha ya kila mtu, itatanda kila mahali kinyume na zamani watu walipokuwa wakitoka mbali na wote wanang’ang’ania Chuo Kikuu cha Nairobi au Cha Kenyatta ambazo ziko Nairobi. Haya ni mambo ya maana. Ninataka kuunga mkono kwamba kila kaunti iwe na chuo kikuu. Nikirudi kuongea kuhusu mheshimiwa marehemu Kijana Wamalwa, alikuwa ametanda Kenya nzima. Kila mahali alikuwa amechukua sifa kwa sababu ya ukarimu na ushujaa wake. Pia kwa sababu ya kubaki na njaa ili kuhakikisha kwamba watu walio mbele yake, wamefaidika. Jambo hili halingefanyika sehemu fulani pekee. Kwa fikira zangu, Bunge lingekuwa na Kamati maalum ambayo itakaa na kuwachagua mashujaa wetu na watu walioleta faida kubwa katika kile eneo la Bunge, ili iweze kuwataja. Hali ya kuwa sehemu fulani tu ndio mashujaa wanatajwa inavunja moyo tukijua kwamba Uhuru wa nchi hii ulipiganiwa na watu tofauti tofauti na kutoka sehemu mbali mbali. Kama vile Pwani, kuna wengi ambao walipigania Uhuru na mpaka sasa, hawajulikani na wamepuuzwa. Kwa mfano, kuna wazee kama vile Salim Mwamgunga na wengine ambao walipigana vikali katika kupatikana kwa Uhuru wa nchi hii. Hawa ni watu ambao pia wangefikiriwa. Kamati ya Bunge ambayo inahusika ingeenda katika kila sehemu ya Kenya ili waweze kujua ni nani aliyepigania Uhuru na akapewa nafasi yake, kuliko kutaja mtu mmoja mmoja. Vile vile, mtu kama mhe. Kijana Wamalwa, sio tu ajulikane kule Kitale kwa sababu ni kwao. Kutokana na ushujaa wake na alivyopigania demokrasia, ni haki yake kabisa atajwe na hata kama ni hapa Nairobi, kutafutwe kitu kimoja kizito kiitwe jina lake. Hiyo Kitale peke yake haitoshi kulingana na kazi nzuri aliyoifanya. Vile vile, ninaona kwamba ni haki yetu hivi sasa tuhakikishe kwamba walio hai pia wafikiriwe mapema ili wakipata ile sifa wajue wameipata na waione. Siyo kumngojea mtu afe ndiyo tumtaje kwamba ni mzuri. Kwa mfano, “Baba” anayo haki kutokana na upiganiaji wake wa nchi hii. Anayo haki ya kutajwa na chuo kikuu kule kiitwe Baba Raila Amolo Odinga Technical University ili apate nafasi yake. Kwa hayo machache, asante sana."
}