GET /api/v0.1/hansard/entries/497721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 497721,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497721/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Njoroge",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13158,
        "legal_name": "Ben Njoroge",
        "slug": "ben-njoroge"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nasimama kupinga Hoja hii inayohusu majina ya Maseneta ambao yameorodhishwa katika Hoja hii iiliyo mbele ya Seneti. Nashangaa ni nini hasa kilikuwa kibaya au ni dosari ipi imetokea katika Kamati ya Kikatiba na Haki za Binadamu inayoongozwa na Sen. Wako. Nikiangalia majina ya watu ambao wameongezwa katika hii Kamati tunayoipendekeza, tisa wamekuwa wanachama katika Kamati ya Sen. Wako. Kama hawakuweza na hawawezi kufuatilia yale mambo yote ambayo yanaendelea kule kortini au kushauri hii Seneti kuhusu maswala ya kikatiba, basi ningependekeza tuwe na mwenyekiti mwingine wa Kamati tunayoipendekeza. Si vyema mwenyekiti wa Kamati ya Maswala ya Kikatiba na Haki za Binadamu aendelee kuwa mwenyekiti wa Kamati hii mpya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}