GET /api/v0.1/hansard/entries/497723/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 497723,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497723/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Sen. Wako, kwa wakati huu, ni mwenyekiti wa Kamati hii. Kwa hivyo, sioni vile Kamati hii mpya itakavyojishughulisha na kusuluhisha shida ambazo tunazo kati ya Seneti na Idara ya Mahakama. Bw. Naibu Spika, kuna Hoja nyingi ambazo huletwa mbele ya Seneti hii. Hii ni kwa sababu kumekuwa na kesi nyingi ambazo zimewasilishwa kortini. Inafaa tujiulize kama Hoja nyingi ambazo tunajadili katika Seneti hii zinamanufaa yoyote kwa nchi hii. Hoja inazungumzia maswala ambayo tayari inashughulikiwa na mawakili wetu ambao wanaheshimika sana. Nilishangaa kumsikia mmoja wao akisema kwamba Kamati hii ambayo tunayobuni leo itapambana maswala ya kisiasa ambayo inaendelea kati yetu na idara ya mahakama. Jambo la kushangaza ni kuwa wengi wa Maseneta ambao majina yao yako katika orodha hii ni kutoka mrengo wa wanasheria. Je, kwa nini hakuna wanasiasa wengi kutoka taaluma zingine ambao wamekwa kuwa wanachama wa kamati hii?"
}