GET /api/v0.1/hansard/entries/497790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 497790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/497790/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nilikuwa ninasema ninapinga kuundwa kwa kamati hii. Hii ni kwa sababu itakuwa ikifanya kazi kama ile inayofanywa na kamati ya Maswala ya Kikatiba na Haki za Binadamu. Ni Maseneta wachache ambao wameongezewa katika orodha hii. Ikiwezekana ni vyema kubadilisha mwenyekiti wa kamati hii tunayoipendekeza. Kamati ya Sen. Wako inawajumuisha wanasheria wengi kama vile Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Sen. Kiraitu Murungi na wengine ambao wanaweza kuongoza kamati kama hii. Kwa hivyo, hata kama Seneti itapitisha Hoja hii, naona kuwa kamati hiyo haitakuwa na manufaa yoyote wala haitaongeza lolote katika Seneti hii. Kama ingewezekana, kamati hii ingekuwa na nyuso geni kabisa ili tuweze kubadilisha yale ambayo tunafikiria yamekuwa yakikwama katika mambo ya kisheria. Kwa hivyo machache, ninapinga Hoja hii. Pia ninapinga mwenyekiti anayependekezwa hapa. Asante sana, Bw. Naibu Spika."
}