GET /api/v0.1/hansard/entries/498667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 498667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/498667/?format=api",
"text_counter": 357,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Pia, naomba kutoa shukurani kwa kamati ambayo niko, ya Afya. Kama unavyojua kesho tunaenda safari ili tujue hali ya kupambana na ugonjwa wa Ebola kwenye mipaka iko namna gani. Maoni yangu pia kwa viongozi ambao tuko hapa ni je: Wangapi ambao ukienda nyumbani, labda wapitia pale hospitali? Ni kama tumeacha zile hospitali bila mwelekeo. Ukienda pale kama kiongozi, wale wauguzi wanajua viongozi wetu watakuja. Kama ni usafi, utawekwa wa hali ya juu. Ni wajibu wetu wote kama viongozi tuige mfanao wa Mama wa Taifa na Kamati hii ya Afya. Lazima, kama umeenda nyumbani, upitie uangalie ni nini kinaendelea katika hospitali hizo na uchunguze vile wagonjwa wanatibiwa. Ukienda nchi kama Botswana, utaona ya kuwa hospitali ambazo zina vifaa muhimu, yaani zina kila kitu kinachotakikana katika uuguzi ni zile ambazo ni za mwananchi wa kawaida. Hapa kwetu, sote tunaenda kwenye hospitali za mabwenyenye. Ni jambo la kuhuzunisha sana. Pia, nilikuwa na maoni yangu kwamba hizi hospitali zinazoitwa Level 5 zingefanywa za wanafunzi kujifunza. Utaona ya kwamba wanafunzi hawa wanapelekwa kwa hospitali ndogo ndogo. Utaona ya kuwa mwanafunzi yeyote ambaye anasomea kiwango fulani cha udaktari ama uuguzi hafuati njia mkato. Utaona kuna nidhamu ya hali juu kwa sababu kuna mwanafunzi ambaye anasomea pale. Pia, utaona kuwa hawakimbi pale kwa sababu kuna mtu ambaye anawachunga. Utapata ya kwamba hatutahitaji pesa nyingi sana kwa sababu wao wenyewe hupewa kiwango kidogo cha pesa kama wanafunzi na tutakuwa na wanafunzi wa kila kiwango; wa mwaka wa kwanza, pili mpaka wa tatu. Hiyo hospitali itakuwa na wauguzi moja kwa moja. Bi. Spika wa Muda, tukiangalia mishahara ya wauguz hawa ni duni sana. Huwezi kufanya kazi na hujui utalipwa lini na utalipa nyumba yako lini au utapanda matatu uende kazini na pesa gani. Yaani una ishi tuu. Ukiangalia hakuna kitu ambacho kiko sawa. Ni dhuluma moja kwa moja. Ukiangalia mshahara hautoshi, ni duni na hujui utaupata lini. Ukiangalia kazini, pia kama muuguzi hauna vifaa. Hauna kitu cha kujikinga na maradhi yoyote, mradi ni shagala bagala----"
}