GET /api/v0.1/hansard/entries/498677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 498677,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/498677/?format=api",
"text_counter": 367,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "awali, lazima tuwe tunapitia kwenye hospitali hizi ili tuwaangalie wagonjwa kama viongozi. Wakati mwingine, unaweza kufungwa bandeji ili uone wale wauguzi wanafanya kazi gani. Pia, unaweza kuvaa bui bui ili wasikutambue na kwa kufanya hivyo, utaweza kujua jinsi watu wako wanavyotibiwa. Ni shida kubwa ambayo tuko nayo lakini kama viongozi tukiungana na ule mwelekeo wa Mama wa Taifa, itakuwa ni vizuri kwa sababu mwelekeo huu umepunga Wakenya wengi. Tukiwa na wananchi ambao hawangaliwi vizuri ki matibabu tutakuwa tumepoteza kwa sababu kazi pia haitakuwa haifanyiki. Mtu akienda kazini siku mbili akiwa mgonjwa, mahali pa kukimbilia ni hospitali. Lakini ukienda hospitali, hautapata madawa. Ukienda hospitali utabebwa na ambulansi ambayo itapiga kelele kote njiani na ukifika kule hakuna mtu wa kukupokea. Tunafaa tuone ni nini tunaweza kufanya katika hospitali zetu. Kama nilivyosema hapo awali, ningependekza watoto wasomee humu kwetu huku wakiwahudumiwa watu wetu. Ajira yao itakuwa chini si kama ya mtu ambaye amefuzu. Tukiangalia, utaona kwamba wauguzi wanadhulumiwa sana. Utakuta mtu amezalisha hata watu 40 kwa siku na anayefaidika ni daktari. Kuna dhuluma ambayo"
}