GET /api/v0.1/hansard/entries/499321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499321,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499321/?format=api",
    "text_counter": 188,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Asante sana mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Mambo ambayo yako mbele yetu ni muhimu sana kwa kila binadamu. Kama tunavyojua kwa kila mtu, maji yakitajwa anahisi kwamba ni kitu ambacho anahitaji. Tukiendelea kuangalia mambo kuhusu maji, ninajua kila mmoja katika eneo la uwakilishi Bungeni la Ruiru anaangalia aone ni kitu gani nitasema kuhusu maji. Lakini shida ya maji iko katika Kenya nzima. Ningependa kuongea kidogo kuhusu akina mama ambao wanasumbuka zaidi na jambo hili la maji. Hata kama tutakuwa tukiyashughulikia mambo haya katika kaunti, ninahuzunika zaidi ni kikumbuka kwamba ukifika katika maeneo ya Ruiru, Mwiki, Githurai na Mwihoko, utakuta akina mama wanachota maji kwa mitungi. Kwa hivyo, masaa mengi yanapotezwa na akina mama wakitafuta maji. Pesa nyingi zinatumika katika mipango hiyo na ni shida kubwa sana pesa hizo kufikia mwananchi wa kawaida. Ninasema kwamba ni vizuri tuwe na wataalamu ambao watasomesha watu kuhusu njia nzuri za kuhifadhi maji, hata kama ni maji ya mvua. Mhe. Naibu Spika wa muda, ninaomba kwa heshima--- Mwenzangu, mhe. Millie Adhiambo-Mabona, ameongea mbele yangu lakini mimi sio yeye. Naomba kwamba, tafadhali hatutaki mipango hii--- Kuna watu ambao tunawahitaji sana sisi ambao tuko karibu hapa; kuna kampuni ya maji ya Nairobi. Kitu ambacho tunacho ni huzuni kwa sababu majina ni makubwa lakini kazi ni kidogo. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ni jambo la kuhuzunisha sana tukisema kwamba tunataka kupitisha Mswada hapa na wale tunaowapitishia, ambao ni wananchi wa kawaida, hata hawafikiwi na maji. Naomba, hata kama tunasema maji yatakuwa yakisimamiwa na kampuni ya maji ya Nairobi, ni vizuri tujue kwamba huko tunakosimamia kunaenda maji kwa mwananchi wa kawaida. Tuweza kuwa na maji katika miji na tunapatiwa maji. Kuna yule ambaye yuko pale mashinani, hata akisikia mkiongea kuhusu maji, machozi yanamtiririka kwa sababu kuyapata maji ni vigumu. Ule mpango utakaopangwa usipangiwe tu kwa wale watu ambao wanaonekana mijini, lakini tuangalie hata wale ambao wako mashinani ndio waweze kufikiwa na maji. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}