GET /api/v0.1/hansard/entries/499322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499322,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499322/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2715,
        "legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
        "slug": "esther-nyambura-gathogo"
    },
    "content": "Pia, tuangalie wakati tunapanga mipango hiyo, isitumie pesa nyingi hata watu wetu wakakosa maji. Sipingi Kampuni ya maji ya Nairobi, lakini nauliza kazi yao katika eneo Bunge la Ruiru ni ipi? Watu wametaabika, na kubeba maji machafu. Watu wengine wameenda kwa mashimo ya mijengo kuchota maji kwa sababu wana shida. Tafadhali, nikiunga mkono Mswada huu, nawaomba washughulikie suala hilo na wajue kwamba mwananchi wa kawaida analia usiku na mchana kwa sababu ya maji. Akina mama wameumia na migongo yao inauma kwa sababu ya kubeba maji. Tafadhali tuongee hapa Bungeni na pia tufikishe maji pale mashinani. Asante mhe. Naibu Spika wa Muda; ninaunga mkono Mswada huu."
}