GET /api/v0.1/hansard/entries/499878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499878,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499878/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii. Kwanza, nataka niunge mkono Hoja hii kwa nguvu zangu zote. Hoja hii imechelewa; ingekuwa imeletwa kitambo na tungekuwa tumewapeleka watu hawa kortini na kumalizana nao. Njama na mbinu zilizotumika kuua Seneti ya kwanza ndizo hizi zinazotumika hivi sasa. Mwaka wa 1965, walianza kusema kwamba Seneti haikuwa na kazi na kwamba kazi yake ingeweza kutekelezwa na Bunge la Kitafa. Wakaanza kusema kwamba lile Bunge la Seneti la kwanza linaweza kufanya kazi yake, lakini iangaliwe na Bunge Kuu. Pia, wakasema kwamba Bunge lile lilikuwa na watu wengi na lilikuwa halina maana ila tu kumaliza pesa za Wakenya. Ukiangalia tunavyopigwa vita sasa, ni kama historia inajirudia; tunaambiwa kwamba kazi ya Bunge hili inaweza kutekelezwa na Bunge la Kitaifa na kwamba Bunge hili linaongezea mshahara na matumizi ya Serikali na kwa hivyo, linaweza kufutiliwa mbali. Lakini jambo ambalo hatuelezwi ni kwa nini Serikali ya majimbo iliuawa mwaka wa 1965. Ni kwamba maseneta waliokuweko wakati huo walihongwa na kupewa viti bila kugombea. Waliongezewa muda kwa miaka miwili na wakapewa marupurupu ndiposa wakakubali kuua majimbo. Lakini Katiba ya sasa ambayo tulipitisha 2010 ilisema wazi kwamba ugatuzi utakuwepo na ndio maana asilimia 80 ya Wakenya waliipigia Katiba mpya kura kwa sababu ya ugatuzi. Bw. Spika tulipounda Seneti kuanzia mwaka jana, tuliona majaribio mengi kwa Bunge hili la Seneti na tukaanza kusikia wenzetu wengine wakisema kwamba wanaweza kutekeleza kazi yetu. Wengine wakasema kwamba uchumi hauruhusu Bunge la Seneti kuwepo; wengine wakasema kwamba Bunge la Seneti ni la wazee lakini ukumbuke kwamba, panapo wazee hapaharibiki jambo. Ndio maana ninasema kwamba Katiba hii ya 2010 iliweka Kenya kuwa na mfumo wa ugatuzi. Bila ugatuzi, hakuna Kenya na bila Kenya, hakuna ugatuzi. Ndio maana wakaweka Seneti kwenye Katiba na wakasema kwamba kazi yetu pia ni kutunga sheria. Lakini hivi sasa, inavyoonekana ni kwamba walivyofanyia Bunge lile la Seneti, wanataka kufanyia Bunge hili. Lakini nataka niwaambie kwamba Bunge hili ni tofauti kwa sababu tuna uwezo, ujuzi, maarifa na malengo. Hatutakubali kamwe mtu yeyote kugusa Bunge la Seneti. Ukitaka kuvunja Kenya, ni lazima uvunje ugatuzi na Seneti. Hii ndio maana magavana wanapoendela kusema kwamba wanataka pesa mshinani, lengo lao la pili wanasema kwamba ni kuboresha Bunge la Seneti liwe na nguvu zaidi kuliko lile Bunge la wengi. Lakini sisi, masikitiko ni kwamba tuliwapuuza na tukawapiga vita; tunatetewa na tunakataa. Ni lini mgonjwa akakataa kutibiwa na daktari? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}