GET /api/v0.1/hansard/entries/499880/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499880,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499880/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Masikitiko ndio hayo. Lakini kwa sasa, kwa sababu tumepigwa vita na tumeamka, ukweli ni kwamba tutaonyesha Wakenya kwamba Bunge hili lina Wabunge wastaarabu wanaojua sheria, lina ujuzi na lina uvumilivu. Tunaenda kutupilia mbali hizi sheria zote zilizopitishwa bila kupitia Bunge hili. Inafaa zirudishwe hapa katika Seneti. Na bila kurudishwa hapa, nina hakika kwamba Korti Kuu inaenda kukubaliana nasi. Bw. Spika, hapa tunapoenda kule mashinani, wao wanajua kwamba Seneta ndio baba wa kaunti na ndio maana wanajua kwamba ugatuzi hauwezi kuondolewa kwa sababu ya Seneti. Tukikubali, ama tuandhaliwe ama tupewe chochote tukiambiwa kwamba Seneti iondolewe, basi wakiondoa Seneti, na ugatuzi utaondolewa. Na mimi ninatoka Taita-Taveta Kaunti. Kwa miaka 50 tangu tupate Uhuru, tulikuwa tunalilia majimbo na sasa tuko na majimbo. Tumepata jimbo la Taita-Taveta. Mkitaka kuondoa ugatuzi, basi kutakuwa na shida nchini Kenya, na itakuwa shida ya kisheria kwa sababu hatuwezi kukubali kwa sababu kwa mara ya kwanza, tumeona Ksh3 bilioni zikiletwa katika kaunti yetu. Hatukuwa tumewahi kuona pesa kama hizo kwa miaka 50. Leo hii, unataka utuambie unaondoa ugatuzi, uturudishe Nairobi kunyanyaswa ili mambo yetu yawe yanajadiliwa hapa na kukubaliwa hapa? Sioni kama Wakenya wengine watakubali. Ndio maana tunasema kwamba Bunge la Seneti litadumu na wasiokubali hayo, basi wakubali hayo. Hawana namna nyingine kwa sababu watashindwa. Ndio maana tunasema kwamba katika sheria zilizoko, tunataka kuungana na magavana wanaosema kwamba Bunge la Seneti liwe Bunge Kuu. Nitawaunga mkono kwamba waongezewe pesa kwa maana sisi ndio walinzi na watetezi wa kusimamia ugatuzi. Wakipata pesa nyingi na wazitumie vibaya, pia wembe ni ule ule; tutawapeleka gerezani. Lakini kwa sasa, ndugu zangu, Maseneta, tukubaliane kwamba Bunge la Seneti ndio Bunge Kuu. Tuungane mkono na magavana ili tuwatetee huku tukijitetea. Na sio viti vyetu pekee bali kwa ustawi wa nchi hii. Tunataka ugatuzi ili Kenya iendelee katika kila pembe. Tunaambiwa kwamba tangu ugatuzi uje, ufisadi umezidi. Lakini sivyo. Kama pesa zinatumika vibaya, ninaamini kuna wakaguzi wa Serikali ambao wanaweza kukagua hesabu na watawashika wezi. Ndugu zangu, tuende kortini, sio tu kwa sababu sisi ni Bunge la Seneti bali tunataka tudhihirishe kwa viongozi wa nchi na Wakenya kwamba huwezi kuichezea Katiba; kuna vipengele na Mahakama ya Juu zaidi ambayo tunaenda kuitegemea. Nina hakika. Na hata ninapolala ninajua kwamba tunaenda kushinda kesi hii asubuhi ili iwe funzo kwa wote ambao wanataka kusema kwamba Seneti halina nguvu, halina kazi na ni la wazee. Sioni kama kuna mzee mkongwe hapa Seneti. Watu wote walioko hapa ni watu wa maarifa. Kuna wanasheria, mahakimu, madaktari na watu wa aina mbali mbali. Hata Bw. Spika ni mtu ambaye amekuwa bungeni kwa miaka 15. Ana ujuzi wa kutosha na ndio maana tunaomba sheria ifuatwe. Kama kuna Mswada unaletwa Bunge na Katiba inasema kwamba Mswada huo ujadiliwe na Maspika wetu wawili, ni lazima sheria ifuatwe. Mtu mmoja asiseme: “Mimi nina ujuzi zaidi kuliko mwingine.” Hata yule bingwa wa ndondi, Michael Tyson, alikuwa anasema ni mbabe lakini akachapwa na mwingine. Kwa hivyo, tunataka sheria ifuatwe. Kama The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}