GET /api/v0.1/hansard/entries/499882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499882,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499882/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "imesemekana Maspika wawili wakae wazungumze, wakubaliane na haikufanyika, sheria zote walizopitisha zirudi tuziunde upya. Bw. Spika, lingine katika ugatuzi ni kwamba tutetee magavana wapate kazi zaidi. Kwa mfano, katika elimu, kuna mahali Kenya ambapo watoto wanasomea chini ya miti sasa hivi. Serikali Kuu inasema tuiachie kazi hiyo lakini mbona haijaifanya kwa miaka 50? Tunataka tuanze kuongeza zile kazi ambazo serikali ya ugatuzi inaweza kutekeleza zaidi. Kwa mfano, elimu na majengo ya elimu ni kazi ambayo serikali za kaunti zinaweza kutekeleza zaidi. Masikitiko ni hayo. Kwa nini Serikali Kuu inaweka pesa katika Wizara kwa mfano Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi au Wizara ya Mazingara, Maji na Mali ya Asili? Pesa hizo zingekuwa zimepelekwa katika serikali za kaunti kwa sababu mambo ya ukulima, maji na afya tayari yanasimamiwa na serikali za kauti. Naomba ndugu zangu, Maseneta, tunapochangia Hoja hii, tuweke wazi na bayana ili Kenya nzima na kila mwananchi ajue kwamba hakuna mahali tunaenda. Tuko hapa na tutakaa."
}