GET /api/v0.1/hansard/entries/499884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 499884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499884/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hatuondoki ng’o! Wale ambao wanasema kwamba wataifanya mambo mabaya ili tuondoke, Bw. Spika, nataka nikuhakikishie kama Seneta wa Kaunti ya Taita-Taveta kwamba upo na utakaa. Ikiwa kuna sheria ambazo zilitiwa sahihi bila kuangaliwa na Seneti, wananchi wa Taita-Taveta wanasema tuzirudishe. Kwa mfano, tukizingatia Mswada wa Madini, Taita-Taveta ni mojawapo ya kauti zenye madini mengi. Je, unasema watu wangu, serikali yangu na mimi nisiwe na la kusema ili Waziri hapa apeane leseni anavyotaka na Serikali Kuu ifanye inavyotaka na wanakuja kuchimba madini kwangu? Haiwezekani na haitawezekana. Nataka Sheria hiyo irudishwe hapa, tuichaingie ili mwananchi wa kawaida ajue kwamba ana usemi kwa madini, maji na hata misitu. Bw. Spika, na ndugu zangu, hata kama ni kuchanga kwa mfuko, niko tayari tutoe pesa, tuende kortini, kesi hii tuishinde ili tuweke alama, na funzo kwa wote kwamba Katiba sio kitu cha kuchezea. Katiba ni kitu cha kutimizwa. Kwa hivyo, naomba ndugu zangu wote tuunge mkono Hoja hii kwa dhati ili tuweke funzo, somo na Seneti – sio hii pekee, bali Seneti zingine – zidumu bila kusumbiliwa na yeyote. Asante Bw. Spika. Naunga mkono Hoja hii."
}