GET /api/v0.1/hansard/entries/499922/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 499922,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499922/?format=api",
"text_counter": 183,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwa moyo mzito sana ninaunga mkono Hoja hii iliopendekezwa kwetu na Kiongozi wa Wengi katika Bunge hili. Ningependa kuyaangazia mawazo yangu juu ya uzembe wa watu fulani ambao kwa hiari yao wenyewe wamekataa kutii sheria na kuhujumu uongozi wa Rais wa nchi hii. Na sijui kama anajua ama hajui. Ni sawa kukosa mara moja au mara mbili, lakini kutia sahihi yake Miswada 46 bila kujali Seneti si jambo mwafaka. Ametia kidole chake bila kuzingatia Kipengele 93 cha Katiba. Kipengele hiki ni juu ya umuhimu wa Seneti katika Miswada yote. Je, mtu huyu ni mbumbu au hekima ilienda wapi? Hiyo ndio picha unayotaka iwe ya Rais wa nchi hii kuwa hatunzi sheria. Aliyeleta Hoja hii amenukuu vipengele 93, 94, 91 vya Katiba yetu ambavyo vinapeana mamlaka kwa korti zetu kuangalia haya mambo. Kipengele 110 cha Katiba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}