GET /api/v0.1/hansard/entries/499924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 499924,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499924/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kinampa uwezo Spika wa Seneti wetu kukaa na kuangalia haya mambo na Spika wa Bunge la Kitaifa. Amenukuu sheria zote na sitazisoma. Lakini kuna sheria moja ambayo nitasoma kuhusu nguvu alizopewa Rais na Katiba. Kipengele 132(2)(a), kinasema kwamba “Rais atafanya hivi”. Haombwi bali anashurutishwa na kuamrishwa na Katiba. Kwamba, ataiheshimu, kuinua na kutetea Katiba hii. Kufuatana na kipengele hiki, kutia Miswada hii kidole chake mwenyewe aidha hakuonyeshwa, hakuongozwa, hakukumbushwa kwa vyovyote vile kabla ya kufanya hivyo. Kwa hivyo, mwenyewe amevunja sheria. Hivyo ndivyo Katiba ya Kenya inavyosema. Yeye mwenyewe aliapa kuilinda Katiba alipopewe kile Kisu cha Mamlaka ya kutawala Kenya. Yeye aliapa kuitunza Katiba ya Kenya kwa mujibu wa Sheria na akaomba Mungu amsaidie. Bw. Naibu Spika, mimi nitasema maneno kinaga ubaga; sitazunguka hapa na pale. Kwa kweli matope yametupwa kwa uso wa Rais wa nchi ya Kenya.Sitasema haya kwa lugha nyingine ili aendelee kudunduwaa. Nitamweleza kinaga ubaga kwamba ameivunja sheria wakati anapofanya hivyo. Hivi sasa, Mswada utoke kwa “Bunge la Chini” kwamba afukuzwe kazi na hayo mambo yafike katika Bunge hili, tutafanya nini? Sasa tunaelezwa kwamba Mkuu wa Sheria hajaona Miswada mingine hapa na ilifika kwa meza ya Rais na akaweka sahihi bila ushauri wake. Naamini kwamba Bunge hilo halina walevi. Yeye amezembea kazini mpaka Rais anapata makaratasi yamerundikwa yakingojea aweke sahihi yake akiamini kwamba Mawaziri wake wameshayapitia. Je, tuanzie wapi kuwafyeka? Kwanza, Mkuu wa Sheria amezembea kazini na anafaa kuacha kazi. Hana sababu ya kutomwambia Rais wa nchi hii vile Katiba inasema. Ni jukumu lake la kwanza kumshauri Rais wa nchi hii. Bw. Naibu Spika, Wabunge wanasema kwamba Seneti hii ni ya wazee. Ni kweli kwa sababu hapa hakukosi hekima. Hata Biblia Takatifu katika kitabu cha Methali inasema kwamba kichwa chenye mvi ni taji la utukufu. Seneti hii tunaonekana kwa njia ya haki kwa sababu tunafuata Katiba ilivyo andikwa na ikapitishwa na Wakenya. Mimi na wenzangu tulisema kuwa kuna vipengele ambavyo ni vigumu kutekelezwa. Majuto ni mjukuu, huja baadaye. Hamkusikia. Kwa hivyo, Katiba itekelezwe vile ilivyo kwa sababu hivyo ndivyo Wakenya waliamua. Kama ni vigumu kuitekeleza Katiba, basi Wakenya wafanye referendum au kura ya maoni . Lakini mambo ambayo tunaongea sasa hivi si magumu kuyatekeleza. Ni uzembe, ujeuri, ufidhuli na ufisadi. Sijui kuna furaha gani au utukufu gani kuivunja sheria ya Kenya kulia, kushoto na katikati. Wabunge wanasema kwamba kazi ya Seneti ni kulialia. Tutalia kwa sababu nchi inatumbukizwa katika kina kirefu sana. Kwa nini tusilie sisi tukiwa viongozi wenye akili timamu na hekima kuu kwamba nchi yetu inaangamia kwa sababu ya watu wachache wasiotaka kuiheshimu Katiba? Hakuna sheria hata moja isiohusu kaunti. Waanze kulia wakisaga meno wakijua kwamba sasa sheria zote wanazozipitisha kule zinahusu kaunti. Kwa hivyo, sheria zote wanazozipitisha kule zitapitia hapa. Sisi ndio wa mwisho. Wasiwe kama nungu ambao wameficha vichwa vyao kwenye mchanga. Huo ndio ukweli. Tumekataa na lazima haya mambo yapelekwe kwa Mahakama ya Juu Zaidi kama Hoja hii inasema. Korti inafaa kutatua janga hii ili tujue ukweli uko wapi na kama Katiba imevunjwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}