GET /api/v0.1/hansard/entries/499926/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 499926,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/499926/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Miswada 46 tayari imekuwa sheria za bandia. Wananchi wa Kenya watalazimika kutumia sheria za bandia ambazo hazikupitishwa kwa mujibu wa sheria. Hicho ndicho kilio. Kisha tunatarajiwa kukaa kitako na tusiseme ukweli. Tulichaguliwa na tukaapa kuitetea na kuilinda Katiba. Hoja hii si ya ya Muungano wa Jubilee au wa CORD. Hoja hii imeletwa ili watu wote ambao wamevikwa taji za hekima waamue. Mimi naomba tukubaliane na yule aliyeleta Hoja hii kwamba wakati umefika sasa. Ukitaka kuukunja mti, ukunje ukiwa mchanga kwanza. Mti huu ukikomaa huenda ukavunjika ikiwa utapenda kuukuja. Tuukunje sasa hivi na si kesho wala mtondogoo. Wanatucheka kwamba sisi ni wazee. Hata hivyo, katika Bunge hilo sidhani kama kuna hata mmoja ambaye hajaoa au kuolewa. Wote wameoa na kuolewa. Kwa hivyo, wote ni wazee. Ni kisa cha kima au nyani kumcheka mwenzake na haoni kundule. Hakuna ambaye hatakuwa mzee siku moja. Lakini tumekubali kwamba wao ni vijitoto visivyo na hekima kwa sababu wamekubali hivyo. Sasa sisi tuwafundishe kwa sababu wamevunja sheria. Tuwatangazie hata kwa kupiga madebe, tarumbeta na ngoma kwamba wamevunja sheria. Tumeamua kuchukua nafasi yao kwa mujibu wa sheria kuongoza nchi hii. Sasa hili ni gurudumu kubwa ambalo limeanza kubingiria; litakata vichaka, vichwa vya watu, mawe na chochote kile kitakacho simama mbele yake. Ninahakika kwamba Mahakama, kama kweli ina watu wasomi ambao wanajua kutafsiri sheria ilivyoandikwa, itakubaliana na mawazo ya Seneti. Je, watapokubaliana na mawazo ya Seneti, ni nani atayefyekwa? Nakubaliana na Sen. Mutahi Kagwe aliyesema kwamba ingekuwa vizuri kama Rais wa nchi angerudisha Miswada 46 aliyoweka sahihi ili kusiwe na aibu kwake. Tunamwambia hivyo kama Maseneta na wala si kama wanachama wa Jubilee au CORD. Hata wale wa muungano wa Jubilee wanamwambia:- “Kiongozi wetu, tahadhari kabla ya hatari.” Lakini asiyesikia la mkuu, huvunjika guu. Asante, Bw. Naibu Spika."
}