GET /api/v0.1/hansard/entries/500130/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 500130,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/500130/?format=api",
"text_counter": 24,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika, ninaomba niheshimu uamuzi wako na mwelekeo wako kwa Bunge. Hata hivyo, mimi ni mwanachama wa Kamati ya Ardhi. Matamshi yangu hayamaanishi kwamba ninaupinga uamuzi wako. Wakati tulipotoa uamuzi wetu, kama Kamati, hatukuwa tumeipata barua uliyoinakili hapa. Kama tungekuwa tumeipata, labda uamuzi wetu ungekuwa tofauti. Kutokana na uamuzi wako, inabainika kwamba Kamati ya Bunge ilienda kinyume na kanuni na sheria za Bunge kwa kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari. Kamati ya Bunge haikuwa na habari kabisa kuhusu waraka huo. Ndiyo maana Kamati ya Bunge imetoa mwelekeo mwingine. Je, hiyo barua ilikuwa wapi? Hayo ndiyo mambo ambayo ningependa yawekwe wazi. Ndiyo maana Kamati ya Ardhi inafikiria kwamba labda kuna udanganyifu fulani ama kuna mambo fulani ambayo yanatokea bila ya kuwepo kwa uwazi. Kama tungekuwa tumeipata barua hiyo, bila shaka uamuzi wetu ungekuwa tofauti. Ninaomba nieleweke na wenzangu kuwa Kamati haikuwa imeipata barua hiyo. Ahsante."
}