GET /api/v0.1/hansard/entries/500746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 500746,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/500746/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Asante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangie Mswada huu ambao umeletwa mbele ya Bunge hili. Ningependa kutoa mifano ya vipengele na maelezo yake ambayo yamenifurahisha katika Mswada huu na sababu za umuhimu wake katika Kenya hii ya leo. Kwanza, kipengele cha tano kinazungumzia uaminifu, uadilifu, uwasi na ufuataji wa sheria ambao unastahilika kwa kila mfanyakazi wa umma. Kipengele cha tisa kinaelezea uwazi kuwa kila mmoja atahukumiwa kulingana na vile ambavyo atakavyokuwa amefanya yeye mwenyewe. Mtu hatakuwa na sababu ya kusema kuwa alifanya vile alivyofanya kwa sababu aliambiwa na mkubwa wake ama alifanya vile alivyofanya kwa sababu aliteleza kwa njia moja ama nyingine. Lakini zaidi ya yote hayo, Kipengele cha 10 katika sheria hii kinaelezea uwazi kwamba kuna ulazima wa kila jamii, kila jinsia, kila kabila na hata wenye ulemavu kuwekwa usawa katika kila usajili na uteuzi wa maswala yenye kuhusiana na sekta ya umma. Nasema kuwa nimependezwa zaidi. Tarehe moja Novemba, katika notisi iliyochapishwa katika Gazeti rasmi la Serikali, Waziri wa Afya alichagua watu 17 kuwa katika bodi ya Medical Practitioners and Dentists Board. Jambo la kusikitisha ni kwamba katika majina hayo 17, matano yalitoka kabila moja na makabila mengine yakapewa watu watatu watatu. La kusikitisha zaidi ni kwamba eneo zima la Pwani halikupata hata mtu mmoja. Eneo la kaskazini mashariki pia hakuna hata jina moja The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}