GET /api/v0.1/hansard/entries/501114/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 501114,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/501114/?format=api",
    "text_counter": 293,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Yangu ni machache. Mambo ya msongamano wa magari katika Nairobi ni makubwa sana na hili linahangaisha wananchi sana. Kwa mfano, ukitumia Mombasa Road, utajikuta umetumia saa nzima na ulikusudia kutumia nusu saa. Lakini kwa saa hii Mhe. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia hiyo Barabara ya Jogoo na ile ya Landhies, na mahali wanasema wanataka shamba la ekari 50, huku ukizingatia kuwa thamani ya ardhi Nairobi ni milioni 400 ekari moja na ukiangalia wote wanaosikika wakiunga mkono Hoja hii, utaona kuwa wote ni (word expunged ) wa mashamba. Kwa sasa, tukipeana nafasi ama tupitishe Hoja hii kwamba tutengeneze hii barabara na hiyo nyingine na uangalie Kenya Railways vile ilivyo kwa saa hii, hilo shamba liko mahali pamoja. Mahali liko, ukiangalia Jogoo Road na Landhies Road, kwani tutabomoa zile ghorofa za Landhies Road ndio tuzipeleke mahali ardhi iko ama hii barabara ya Jogoo Road kutoka Outer Ring tutaivuta kutoka Railways ipelekwe Jogoo Road ndio iweze kufidiwa? Ndio maana ninasema kuwa huu ni (word expunged ) mtupu! Jambo lingine ni hili Mhe. Naibu Spika wa Muda, mambo ya Tigania East ni ya Mpuru M’Aburi; mambo ya Starehe ni ya Mhe. Kamanda. Kwa nini unasikia Mheshimiwa anatoka pembe ile nyingine anakuja kupanga mipango ya eneo Bunge lingine? Mhe. Kamanda mwenyewe amesema kwamba kule hiyo ardhi haitoshi, hii ni kumaanisha ya kwamba hili ni kundi kama lile lilipangwa kule Karen. Huu ni ( wordexpunged ) mtupu. Huu ni (word expunged ) wa wizi na hizi ni nyumba za Kenya Railways wanataka kubomoa."
}