GET /api/v0.1/hansard/entries/501373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 501373,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/501373/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Kabla Mswada huu haujawa sheria itakayopitishwa na Bunge hili, nitaliuliza na kuweka wazi katika Bunge jambo hili ili waziri aweze kujibu kwa nini akawachagua watu bila kufikiria wengine. Alivunja Katiba ya nchi hii alipofanya hivyo. Mwishowe, kuna kipengee cha 14 ambacho kinaeleza kuwa kila sekta ya umma itaweka orodha ya kila mtu anayeletewa lawama dhidi yake, ama dhidi ya sekta fulani ya umma. Ndugu yangu alizungumza hapa mbeleni na akataja kwamba hivi majuzi alienda katika afisi za kutoa paspoti za Kenya. Alieleza kuwa kwa muda wa masaa machache alipata paspoti yake. Nataka kumkumbusha kwamba hata mimi katika muda wa masaa kadhaa nilipata paspoti yangu. Sababu ni kwamba sisi ni wabunge. Hatuko hapa kwa sababu ya kujitetea sisi wenyewe, lakini tuko hapa kwa sababu ya kuwatetea watu walio mashinani. Kuna fununu kwamba Idara ya Uhamiaji ina nia ya kufunga afisi zake katika eneo la Mombasa, jambo ambalo halijafika rasmi katika Bunge. Hilo likifanyika, bila shaka maelfu, au mamilioni, ya watu watateseka. Tunaiomba Idara ya Uhamiaji kabla wakati haujafika wa kupigana na kuelezeana, itakuwa sawa kama kuna shida itatuliwe kabla ya jambo lolote lingine. Sheria hii itatusaidia sisi hususa watu wa Pwani kwa sababu kama kuna kitu chochote ambacho kinawatesa watu ni suala la vitambulisho. Unaweza kufika katika afisi ya vitambulisho na una kila kitu chako--- Nasikitika sana kwamba hivi juzi kuna mzee mmoja wa mtaa ambaye alipoteza kitambulisho chake, lakini watoto wake wote wana vitambulisho vya Kenya. Alipoteza kitambulisho chake na hana nakala ya kitambulisho hicho. Leo ana miezi minane hajapata kitambulisho kingine kwa sababu anaambiwa kwamba yeye si Mkenya. Haya ndiyo mambo yanayojiri katika mitaa na miji yetu. Tukiwa hapa kutetea haki za umma wasiojiweza na walala hoi, lazima tukubali Mswada huu upite ili kila mwisho wa miezi mitatu, miezi sita au mwaka mmoja, tuwe tunajua hatua mwafaka zitakazochukuliwa dhidi ya kila sekta iliyoelekezewa kidole cha lawama kwa kuwatesa wananchi kwa kutojua ama kwa kusudi. Asante sana mhe. Naibu Spika. Nina imani kwamba yale makosa yanayoendelea kufanywa yatarekebishwa kabla hatujaanza kupambana na wale wenye kusumbua watu wetu. Asante."
}