GET /api/v0.1/hansard/entries/501931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 501931,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/501931/?format=api",
    "text_counter": 254,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii kuweza kuunga mkono taarifa hii inayopendekeza kwamba Dr. Lydia Nzomo aweze kuchukua nafasi ya uwenyekiti wa Tume ya Walimu. Mama ameonyesha ujuzi na tajriba nyingi katika kazi yake tangu alipoajiriwa. Rekodi yake, ukiifuatilia kwa umakini, utaona ya kwamba hakuna kashfa katika kazi zake zote zile alizoendelea nazo kwa miaka 23 katika TSC. Ni dhahiri kwamba tumechelewa kumpata mama huyo ambaye tunatarajia aweze kuiongoza TSC vyema. Katika mahojiano, aliweza kuelezea ya kwamba atafanya lipasalo lolote lile kuona ya kwamba walimu wanafidiwa kisawasawa. Hilo ndilo jambo ambalo hakika kwa wakati huu limekuwa donda sugu. Kila wakati ni kana kwamba Serikali haifahamu kitu kwa maana ni lazima walimu wagome ndipo waweze kuongezewa mshahara. Lakini ameahidi ya kwamba hakutakuwa tena na mambo kama haya ya waalimu kugoma ndipo waongeze mishahara. Atajaribu kadri ya uwezo wake aweze kuona ya kwamba anahusisha wale wote wanaohusika kuona ya kwamba mishahara ya walimu inawekwa kisawasawa. Na vile yeye mwenyewe amekuwa mwalimu, anaelewa dhahiri ni wapi panaposumbua zaidi. Ni wapi mwalimu anabanika zaidi. Vile vile, kuna sehemu ambazo zinastahili kulipa malipo yale ya ziada kwa sababu ya zile shida zinazopatikana kule lakini kwa wakati huu TSC imeziondoa. Hizo pia, ni ahadi yake kuwa atajaribu kuangalia na kuona ya kwamba walimu wale wanarudishiwa marupurupu yao kama ipasavyo. Hakuna mwingine kama yeye. Isitoshe, kiti hiki cha uwenyekiti wa TSC ni miaka mingi kimekaliwa na wanaume. Wakati umefika sasa wa mama kutuongoza. Asante kwa hayo."
}