GET /api/v0.1/hansard/entries/502065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 502065,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/502065/?format=api",
"text_counter": 388,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Machira",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 769,
"legal_name": "Jane Agnes Wanjira Machira",
"slug": "jane-agnes-wanjira-machira"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mhe. Shebesh katika hili jambo. Jambo hili lilituweka katika picha mbaya sana kama kina mama. Pia limeweka picha mbaya zaidi kwa wazee; hata Wabunge walio katika Bunge hili, picha yao itachukuliwa kama wazee ambao wana picha kama ile ikiwa hawataunga mkono huu mjadala. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni kiazi gani cha nguo ama ni urefu gani wa nguo ambao kina mama wanahitajika kuvaa? Ikiwa kuna urefu wowote, basi hatuwezi kuelezwa na makanga . Ni sisi Wabunge ambao tunapaswa kupitisha sheria hiyo. Ni wanaume wangapi leo wanavaa suruali ambazo ni nusu mlingoti? Washavuliwa suruali hizo na mtu yeyote na wanatuonyesha uchi? Ni wanaume wangapi leo wamebaka kina mama wazee na watoto wa hadi miaka miwili? Wameona wapi uchi wa huyo mama ambaye ni mzee na mtoto wa miaka miwili? Tunataka tuelezwe sisi kina mama tutapitia wapi ikiwa tutaishi tukiogopa katika Kenya hii? Kila siku tunapotembea tunaogopa. Sisi kina mama ni kama tumetengwa wakati wowote ule. Tukienda mtaani ni kina mama, tukienda wapi ni kina mama. Mnataka tufanye nini ili tuwe tunafurahisha? Wazee ambao wako katika vituo vya magari hawaogi na hawatumii maji. Hawasafishi hata wake wao na wanataka kuona sura ambazo zimesafishwa vizuri ili wafurahi."
}