GET /api/v0.1/hansard/entries/502078/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 502078,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/502078/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms) Mumo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 808,
        "legal_name": "Rose Museo Mumo",
        "slug": "rose-museo-mumo"
    },
    "content": "42 Tuesday 18th November, 2014 wetu mahali wanatembea. Waliofanya kitendo hicho, ni kitendo cha kusikitisha sana. Ni kitendo cha aibu na ndio maana nimesema nichangie kwa Kiswahili wale ambao wako kwa lugha hii ya Kitaifa waweze kuelewa ya kwamba akina mama mioyo yetu inavuja damu kwa kuona watoto wetu wakitendewa vitendo vya unyama ambavyo ni vya kuvuliwa nguo. Ni kama tabia zimeanza kuzorota ama tabia zimeanza kuharibika. Labda inaweza kutokana na ulezi mbaya wa hawa watoto. Kama inavyokusudika ni kwamba mwanamke anafaa kuvuliwa nguo mahali ambapo ni ndani ya chumba kama anaangaliwa na daktari hospitalini ama ni mume wake anamtoa nguo lakini sio kumtoa nguo barabarani. Hii ni kuonyesha ya kwamba tabia imeanza kuharibika. Jambo hili tunalilaumu kabisa na tunasema ni vibaya na tunasema likome. Wanawake wapewe heshima kwa maana msichana huyo aliyetolewa nguo, kesho atakuwa ni mama ya huyo anayemtoa nguo. Kesho ataweza kuwa pia ni dada wa mwingine. Ni vibaya kwa maana hao wanaotoana nguo wajue ya kwamba pia watakuwa na wasichana wao. Na sijui kama vile wenzangu wamechangia ni vipi ambavyo mtu anafaa kuvaa? Ni vipi ambavyo mtu anasema ni fupi na nyingine ni ndefu? Wanaume huvaa nguo vibaya. Wengine kama vile mwenzangu Mheshimiwa amesema, wanavaa suruali zinateremka lakini hatushughuliki na wao. Wengine wanavaa suruali zimewabana kabisa na unaona anatembea na akina mama hatushughuliki na wao. Basi ningesema ya kwamba mabinti zetu hata kama tunaona wamevaa nguo vibaya, kidogo tunasema kwamba wana masikio, waelezwe kwa maana nchi ya Kenya ni nchi ambayo iko huru. Nashukuru Makamu wa Rais ambaye alisema ya kwamba watu hawa washikwe. Ninaamini ya kwamba kama wenzangu ambao walitangulia kusema ya kwamba ikifikia siku ya Ijumaa, tuweze kusikia ya kwamba wameshikwa wawili ama watatu na wamefunguliwa mashtaka. Tutashukuru sana kuona ya kwamba hatua hii imechukuliwa kwa vikali kabisa na ningependa tukiwa kama akina mama tupewe heshima kwa maana akina mama ni watu ambao wanapendeza sana wakiwa katika dunia hii. Bila akina mama, dunia haiwezi nzuri. Kwa hivyo, tupatiwe uhuru wa kutembea na kufurahia maumbile yetu na jinsi ambavyo tunavaa nguo. Asante sana; naunga mkono mada hiyo."
}