GET /api/v0.1/hansard/entries/502335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 502335,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/502335/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chiaba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 3,
"legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
"slug": "abu-chiaba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, asante sana kunipa nafasi niungane pamoja na wenzangu na vile vile kuchukua nafasi hii kumshukuru Kiongozi wa Wengi, Sen. (Prof.) Kindiki, kwa kuleta Hoja hii ambayo ina umuhimu sana kwa kulinda haki ya kikatiba ya Seneti. Tumevumilia kwa muda mrefu, karibu sheria hamsini zimepitishwa na Nyumba Ndogo, National Assembly, na kutiwa sahihi na Rais, kinyume na Katiba. Ilikuwa ni wajibu wa Spika wa National Assembly kushauriana na ndugu yake, Spika wa Seneti, ili waweze, kufanya chombo ambacho kinaitwa consensus na kama sheria hizo zinaambatana na devolution ama kulinda haki ya county government ama countyassembly. Hivi sasa Katiba yetu inatupa haki ambayo watu walikuwa wamenyimwa kwa siku nyingi lakini sasa inapatikana. Kama Kaunti ya Lamu haijapata maisha yake kwa miaka hamsini kiasi cha fedha cha Ksh1.7 bilioni. Ingawa pesa hizo hazitoshi lakini inaonekana ya kwamba kazi inafanyika. Hivi sasa katika Kaunti ya Lamu, kuna miradi mikubwa ambayo inafanywa bila kuhusisha watu na Seneti ambayo inalinda haki ya devolution, hizo sheria si za halali. Tunaomba Mkuu wa Sheria anapowasilisha sheria kama hizo kutiwa sahihi amwambie Rais wetu aangalie kama kuna kile cheti ambacho kimewekwa sahihi na Spika wetu wa Seneti na Spika wa National Assembly. Sisi tutakuwa hapa na wala hatutakubali hii Seneti iwe kama ile ya 1963. Wakati huu, kuna maprofesa ambao wamejitolea, kuna watu ambao wamesoma kupindukia na wako tayari kulinda Seneti iwepo kwa damu. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}