GET /api/v0.1/hansard/entries/502792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 502792,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/502792/?format=api",
    "text_counter": 379,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "watu wanachukua muda mrefu sana. Leo asubuhi, nimelala nikifikiria kwamba hali itakuwa ile ile, lakini nilipopata teksi kuja hapa, imenichukuaa masaa matatu na nusu. Nilipochukua taxi kuja huku, nilichukua masaa matatu na nusu; jambo ambalo limenisikitisha sana. Kwa hivyo, Hoja hii haihitaji mjadala kwa sababu ni Hoja ya maana. Ni jambo ambalo linafaa kushughulikiwa na Serikali haraka sana ili tuhakikishe kwamba barabara hiyo imepanuliwa na kuondoa madhara mengi. Kwenye msongamano, watu wanabakurwa vipochi. Wengine wanavutwa, skati zao zinatolewa kwa sababu mhalifu amejificha mahali penye watu wengi ambao wamesongamana mahali pamoja. Mtu huyo anapenya bila kuonekana. Jambo hili likitekelezwa, madhara haya yote yatakwisha. Pia, jambo hilo lisitekelezwe hapa Nairobi tu kwa namna imezungumziwa na mheshimiwa. Inaonekana kwamba idadi ya watu inaongezeka maradufu kila kukicha. Kwa hivyo, kuna haja ya Serikali kuelekeza juhudi hii kwengineko, kama vile Kwale, ninakotoka; kule Malindi kulikotajwa na mhe. Gunga, Ukunda, Msambweni, Rabai na kwengineko ambako idadi ya watu imeongezeka maradufu. Hali tunayoishuhudia katika barabara ya Jogoo itashuhudiwa katika sehemu nilizozitaja baada ya muda mfupi. Ni maoni yangu kwamba Bunge hili liiunge mkono Hoja hii ili tuweze kupata nafasi ya kusafiri kwa urahisi na kufika tunakoenda kwa haraka. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}