GET /api/v0.1/hansard/entries/503505/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503505,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503505/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Nataka kuchukua nafasi hii ya kipekee kutoa rambirambi zangu kibinafsi, familia yangu na watu wa Taita Taveta Kaunti, kwa familia, ndugu na marafiki wa Seneta aliyetuacha, Sen. Kajwang. Kufikia jana tulikuwa na Sen. Kajwang. Tulikutana naye katika lifti ya Kenyatta International Convention Centre (KICC) na tukazungumza. Alikuwa mcheshi kama kawaida na kwa utani akaniuliza, “Mbona ndugu yangu siku hizi umekuwa fiti umepunguza mwili”? Nikamwambia “Ninaenda gym, na wewe pia kitambi kimezidi ninataka ujiunge na mimi ili twende kwa mazoezi pamoja.” Sikujua ya kwamba utani ule sitaupata tena. Sen. Kajwang sasa ametuacha. Pia nataka kuchukua nafasi hii ya kipekee kusema kwamba nilipoingia katika siasa, na hasa chama cha ODM, mmoja wa wale tulifanya kampeini na kutembea pamoja ni Sen. Kajwang. Yeye alikuwa wa kwanza kuzungumza katika mikutano yetu yote ya kisiasa. Aliweza kushangiliwa sana na wananchi alipozungumza. Yeye alituonyesha njia ya kisiasa. Katika Seneti hii, Sen. Kajwang alikuwa mmoja wa wale Maseneta walio na ujuzi wa kuzungumza, kutafakari na kutoa maelezo yake katika ufasaha. Hata katika hali yake ya kuzungumza na kutoa mada, hakuna Seneta mwingine katika Bunge hili aliyekuwa maarufu na waandishi wa habari kama yeye. Kila alipotoa Hoja, ilinakiliwa na ikatolewa katika hali ambayo hakuna Seneta alipata nafasi kama ile. Kwa kweli, tunaweza kusema kwamba alikuwa anaelewa lugha ya Kiingereza. Maneno yake yalikuwa ya kuvutia, si tu kwa waandishi wa habari mbali wananchi wote kwa jumla. Mimi nilikuwa na uhusiano wa karibu sana na Sen. Kajwang. Kati ya Maseneta 67 walioko hapa, Sen. Kajwang alikuwa ni mmoja wakiwa na Prime Minister katika Bunge la Kumi waliokuja katika kijiji changu; pahali nimezaliwa kule Taita Taveta. Niliposikia kwamba ametuacha, watu wengi walipiga simu kutoka nyumbani ili wajue ukweli. Na kwa niaba yao, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa mke wake, watoto wake na watu wa Homa Bay na Kenya nzima kwa kumpoteza shujaa wa kisiasa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}