GET /api/v0.1/hansard/entries/503507/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503507,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503507/?format=api",
    "text_counter": 73,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Alipotembea popote pale, alijulikana kama “bado mapambano.” Haya yalikuwa mapampano ya kisiasa. Lakini ajabu ni kwamba mapambano yake hayakuwa ya kutumia nguvu. Mapambano yake yalikuwa ya kutumia mdomo. Alipomaliza kuzungumza bado mngesalimiana kwa furaha. Alionyesha kwamba alikuwa amekomaa kisiasa. Hata tulipokuwa hapa tukilumbana, tukitoka hapa kwenda kunywa chai, kila mtu alikuwa anamkumbatia Sen. Kajwang. Naomba kwamba tufuate mfano wa mwenda zake, Sen. Kajwang. Ni lazima tujue ya kwamba siasa si uadui wa kijamii. Tunatofautiana tu katika mirengo, dhamira na mipango yetu ya vyama vyetu. Lakini kama Wakenya tuna undugu wetu. Bw. Naibu Spika, katika stesheni za redio za Kenya Wakenya wametuma rambi rambi zao kutoka pembe zote za Kenya wakisema kwamba alikuwa ni shujaa, bingwa, mtetezi na shupavu, hasa kwa kutetea maslahi ya wale ambao walikuwa hawana sauti ya kufika mahali kama hapa. Hii ndio maana akipita popote watu walikuwa wanamuita mapambano. Alikuwa hana daraja. Yeyote awe mkubwa au mdogo alikuwa na kipawa. Alikuwa anaweza kuongea na yeyote. Kwa hayo, Bw. Naibu Spika, Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi hadi siku ya kiama tutakapokutana baada ya sisi sote kuondoka duniani."
}