GET /api/v0.1/hansard/entries/503511/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503511,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503511/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Sen. Kajwang akiwa Seneta wa Homa Bay, nami nikiwa Seneta wa kaunti jirani ya Migori - Nyanza Kusini ni Homa Bay na Migori. Jirani humchagui; ni wa lazima. Unaweza kuchagua rafiki. Nyanza Kusini, tumempoteza kiongozi mashuhuri. Tumempoteza mmoja wetu. Kilio kingemleta. Lakini basi ni hivyo, ni kudura ya Mungu. Jana nikiwa kwenye Kiti cha Spika nimeisikiza hotuba ya Kajwang baada ya kukazana kupata muda kutoka kwangu. Kwanza alikuwa na kadi ambayo haikuwa yake na nikamuuliza Temporary Three ni nani? Akasimama na kutaka kuanza kuongea na nikamkatisha. Ulipofika muda nikamuita Sen. (Dr.) Khalwale kuongea kabla yake, niliona amekasirika kwa sababu alikuwa anataka kuongea. Punde si punde, Sen. (Dr.) Khalwale alipomaliza kuzungumza sikufuata desturi ya kusema kuwa mmoja akiongea upande huu, nafasi inapewa upande ule mwingine. Nilipoona kuna jambo linalomsumbua, nilimpa nafasi. Kwa hivyo, nilipeana nafasi mbili upande huu kwa muda huo. Sen. Kajwang akaanza kuongea mambo mengi ya ajabu niliyoyasikiliza nikiwa Spika wa Muda. Ambalo sikufahamu ni kwamba ilikuwa hotuba yake ya mwisho niliyokuwa nikisikiliza. Bw. Naibu Spika, hata hivyo, alikuwa mtu wa ajabu na mwenye heshima. Sen. Kajwang ni rika yangu; usione nywele nyeupe--- Lakini ananishinda kwa siku kumi kwa umri. Alizaliwa tahere 26 Mwezi wa Saba na mimi nilizaliwa tarehe kumi Mwezi wa Nane, mwaka huo huo aliozaliwa. Alinishinda kwa mwezi mzima. Hata hivyo nilimtishia nikamwambia kwamba: “Wewe, sikukuambia kwamba usiwe na nywele nyeupe, utanisalimu “shikamoo” kwa sababu ni desturi ya Kiafrika”. Alifanya hivyo tangu mwaka wa 2002 tulipokutana nilipokuja Bungeni wakati yeye alikuwa amehudumu kipindi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}