GET /api/v0.1/hansard/entries/503513/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503513,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503513/?format=api",
    "text_counter": 79,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kizima. Tumekuwa pamoja kutoka Bunge la Tisa akinisalimu “shikamoo” hadi jana alipofariki. Alikuwa wa ajabu. Katika Kaunti ya Migori tumemkaribisha sana Sen. Kajwang kwa mikutano mingi na desturi yake ya wimbo. Tutakosa ucheshi wake na sera zake za kutumbuiza. Hata hivyo, alikuwa akiongea mambo yake kinaga ubaga, hakuficha chochote. Sasa tunamuuliza Mungu: Je, mbona janga hili la kifo ambapo tumempoteza Seneta wa pili, na ajabu kutoka kwa “mlango” wa CORD? Sisemi kwamba kifo kiende kwa mlango mwingine. Kiishie hapo. Ninamuomba huyo malaika aondoke. Ashindwe! Aachee Seneti hii kabisa. Majonzi haya ya kila mwaka sisi hatuyawezi. Ingekuwa jambo la kutumia hirizi tungeweza lakini haya ni maumbile na siri ya Mungu mwenyewe. Kifo ni siri tusiyoweza kuitegua. Je, tufanye nini sisi ili tumfukuze huyu malaika mbovu kutoka kwa Seneti hii? Ni maombi tu. Bw. Naibu Spika, tunapowafariji jamii, kutoa majonzi na tukilia kwa vishindo, tunamuomba Mungu amjalie na kumponya babake ambaye alipokea habari hizi kwa kishindo. Ni jambo la huzuni muno kiongozi anapopata matatizo yoyote, iwe ni ajali au kifo, na vyombo vya habari kupeperusha habari hizo hata kabla ya jamii ya kiongozi huyo kuandaliwa kuzipokea. Nafikiri hivyo ndivyo ilivyokuwa mpaka mzee kajipata hospitalini."
}