GET /api/v0.1/hansard/entries/503519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503519/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi hii. Ningependa kutuma rambi rambi zangu na Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o ambaye yuko Uingereza. Alituma rambi rambi zake kupitia kwa Sen. Wetangula lakini alisahau kuzitoa. Kwa hivyo, natuma rambi rambi hizo kwa jamaa, marafiki wote na Seneti hii. Bw. Naibu Spika, mpaka sasa siamini jambo lililotokea. Wakati mwingine nafikiria kuwa ninaota. Hii ni kwa sababu jana tulikuwa na Sen. Kajwang hapa na tukaondoka pamoja. Tulikubaliana kukutana naye, Sen. Orengo, Sen. Ongoro na mawakili wetu ili tuzungumzie kesi zinazotukabili, zinazohusu matumizi ya lugha ya uchochezi na chuki. Tulimngojea lakini hakufika, licha ya wengine wote kufika. Leo niliamka mapema kwa sababu nilikuwa na mkutano saa moja asubuhi. Nilipofungua redio nilisikia kwenye muktasari wa habari kwamba Seneta wa Homa Bay, Sen. Kajwang, alikuwa ametuacha. Nilishindwa hata kuwapigia Maseneta wenzangu kuwauliza kama wamesikia habari hiyo. Niliduwaa na nikawa sijielewi. Baadaye niliweza kuthibitisha kwamba Sen. Kajwang alikuwa ametuacha. Kwa kweli maisha ni mafupi muno. Hakuna mtu anayeweza kusema kwamba ataishi kwa siku ngapi. Kuna vitu viwili kuhusu binadamu. Kuna mwili na uhai. Uhai ndio wenye mwili na mwili ndio wenye uhai. Lakini anayechukua uhai ni mwingine. Kama Mkristo nilifikiria vile Yesu alibemba mizigo ya wenye dhambi hadi kaburini. Sen. Kajwang anaelekea kwenye kaburi sasa akiwa anabemba matatizo na uchungu wa Wakenya. Nasema haya kwa sababu Yesu alisulubishwa msalabani kwa sababu alitetea haki za watu na alitaka kuwakomboa. Sen. Kajwang anaenda kaburini akiwa na kesi ambayo inamngojea kortini kwa sababu alisimama Uhuru Park na kusema kwamba anataka Wakenya wakombolewe na wapate haki zao. Ni Mungu tu atakayeutua mzigo huo na kumlipa kulingana na malipo anayostahili. Tungependa hata wale ambao wametushtaki kwa sababu tunasema kwamba tunataka kuwe na usawa wa Kenya watupumzishe ili tusiende makaburini tukiwa na kesi zinazotukabili."
}