GET /api/v0.1/hansard/entries/503524/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503524,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503524/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, naomba sote tuongee ukweli hapa. Hakuna mtu aliyesimama na kusema kwamba Sen. Kajwang alisema mambo ya chuki au kuwagonganisha au kuwatofautisha Wakenya. Sisi sote tumesema kuwa alikuwa mtu wa kufaa na hata akabuni wimbo wa “bado mapambano.” Kweli nimeshangaa kuwasikia hata wale ambao waliukashifu wimbo huo hapo awali wakisema kwamba unafaa. Kwa nini haukumwambia Sen. Kajwang akiwa hai kwamba huo wimbo wake wa unafaa? Yeye anaelekea kaburini akidhani kwamba wimbo wa “bado mapambano” ni dhambi kuu katika taifa letu. Tuwe wenye haki na kumheshimu Mungu aliyetuumba. Kwa sababu Sen. Kajwang ametuacha nipende mimi nilivyo. Kama unajua kwamba ninafanya mambo mazuri na hutaki kunisifia, unafaa kuaibika."
}