GET /api/v0.1/hansard/entries/503560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503560,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503560/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kama ni kumhonga, tumemhonga”. Tulicheke sana kiasi kwamba Naibu Spika wa Muda, Sen. (Dr.) Machage, akamwona Sen. Mungai kwa sababu alipata kwenye bar bila kubow. Akaniambia unaona mzee mwenzetu anaona mpaka mtu ambaye haku bow pale. Bw. Naibu Spika, hayo ni maneno tuliyoyazungumza na mwenda zake. Tulizungumza kinaga ubaga kama watu wazima na kama wazee. Kwangu mimi na familia yangu, ni pigo kubwa kwa kukosa rafiki ambaye alikuwa mmoja kati ya marafiki muhimu. Busara zake zilikuwa za muhimu sana. Pia, alikuwa mtu wa umahiri kiasi kwamba akiamini jambo, anasistiza nalo. Pia, alikuwa ni mtu mcheshi. Alikuwa anaweza kuzungumzia swala lolote katika hali ambayo utafurahi. Ndio maana aliweza kujulikana kama “Bado mapambano”. Nitakosa ucheshi wake mimi kama Seneta mwenzake. Yeye ni mmoja wa nguzo muhimu sana kwa sababu wakati wowote ambapo unataka ushauri kwake, alikuwa anakupa ushauri katika njia za kitaalamu. Angekupa ushauri kuhusu Kanuni za Bunge kama anavyoelewa na si kama unavyotaka. Ni watu wachache wako hivyo. Wengi hujisemea wanavyotaka na wala sio vile wanavyoelewa. Kwa hivyo, ni huzuni kubwa kumkosa mtu wa aina hii. Waliovyosema Maseneta wengine, naiombea roho yake ikae mahali pema peponi."
}