GET /api/v0.1/hansard/entries/503571/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503571,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503571/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwa niaba ya familia yangu na watu wa Kilifi ningetaka kutoa rambi rambi zangu kwa watu wa Mbita Constituency, vile vile watu wa Kaunti ya Homa Bay na Wakenya wote kwa jumla kwa sababu ya kupoteza kiongozi wao. Tukisema “kiongozi wao” ni kwamba ndugu yangu, Sen. Kajwang, hakuwa mwanasiasa wa Homa Bay peke yake; alikuwa mwanasiasa wa Kenya na alijitambulisha kwa ushupavu wake katika mambo ya mijadala. Alikadiria ushupavu wake katika ulingo wa siasa kwenye jukwaa. Nikisema hivyo ni kwamba Sen. Otieno Kajwang alikuwa mtu mshupavu kwa kueleza sera zake. Sisi katika jukwaa la siasa mara nyingi tulikuwa tukimfananisha. Nikisema hivyo, zaidi sana, nitachukua mfano wangu mwenyewe wa kuweza kumuiga na kusema ya kwamba wakati tulikutana hapa Seneti nilipochaguliwa, kwamba akitengeneza sheria zake za kuwasaidia watu wa Homa Bay na mimi nitakuwa upande huu nikitengeneza sheria zangu za kuwasaidia watu wa kaunti ya Kilifi. Kwa hivyo, ningetaka kusema kwamba alikuwa kielelezo kwa watu wanaotaka kuwa wanasiasa, kwa vijana ambao wanataka kuwa wanasiasa na pia kielelezo kizuri cha sisi wenyewe kama wanasiasa katika nchi ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, nataka pia nikumbuke ya kwamba hivi majuzi mwezi uliokwisha, tuliweza kusafiri naye hadi kule China na wakati tukiwa kule China, wao wanakula chakula chochote, nilimuuliza wakati mmoja kwamba hii nyama ambayo inakaa imenyooka sana ni ya kawaida ama ni nyama ya aina gani? Aliniambia kwamba hiyo---"
}