GET /api/v0.1/hansard/entries/503576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503576,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503576/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "“Ukija China na upate wanakula nyoka, wewe pia kula nyoka, na kama wanakula vyura, wewe kula vyura, maanake tumekuja huku tujue jinsi ya kuishi ili tukirudi nyumbani tuilinganishe na food security yetu”. Kwa hivyo, katika harakati zake za maisha, alikuwa mcheshi na mtu mwenye kufahamu mambo mengi. Ninakumbuka pia wakati fulani tulipokuwa naye kule India, tukiwa katika hali ya kutembea hapa na pale kutafuta medical examination, alitueleza kwamba yeye hawezi kufanya medical examination kwa sababu itamwambia mambo mengi ambayo yeye hakutaka lakini tulimsihi afanye na hatimaye alikakubali kuangaliwa na madaktari. Natoa rambi rambi zangu."
}