GET /api/v0.1/hansard/entries/503601/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503601,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503601/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Pia, natandaza wingu la simanzi hapa Seneti. Kazi ya Mungu haina makosa. Ule ucheshi, umahiri, sifa, na haiba yake Sen. Kajwang hatuwezi kusahau. Ni huzuni kubwa. Niliona ujumbe wa 411 lakini ni kama kichwa changu hakikukubali kuwa ni Sen. Otieno Kajwang. Nilipokuja Seneti leo na kuona picha ya Seneta Kajwang, nilipata huzuni kubwa sana. Niliona sasa ni kweli kuwa kifo kimetupokonya mtu mahiri na shujaa. Kifo kimetuleta pamoja na wale wa upande mwingine, na sisi wa huku Serikalini ndio tumesikia majonzi makubwa kwa sababu pale ninapoketi, Bw. Spika wa Muda, ni upande wa pili kabisa. Kwa hivyo tunapokaa upande huu wote twaona Sen. Kajwang. Heri wale wenzetu ni kama wako kwenye bus, wanaenda safari na Sen. Kajwang amekaa nyuma. Upande huu sisi tumejawa na wingu la simanzi kabisa. Mswahili anakwambia; nyoko nyoko ni kuonana. Kwa hivyo, ile nyoko nyoko ni ile kuonana. Sasa yale mambo yote tulikuwa tunaona Sen. Kajwang labda hivi ama vile, saa hii ndio tumejua kuwa kweli kifo ni kitu ambacho huwezi kukirudisha nyuma. Watamani awe yupo na umwite “Bado mapambano” naye anakwambia “kabisa.” Bw. Spika wa Muda, ni huzuni kubwa kwa watu wa Homa Bay, nawapa pole za dhati. Kwa watu wa Seneti, pole, naomboleza nanyi. Tuko pamoja na tusimkosoe sana Mwenyezi Mungu. Tumwombeni Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema peponi. Mwenyezi Mungu amlaze pale ambapo yeye mwenyewe awepo kwa sababu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}