GET /api/v0.1/hansard/entries/503734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503734,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503734/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Spika. Nami pia nataka kutoa risala zangu za rambirambi kwa jamii ya Senator Otieno Kajwang’, seneta wa Homa Bay, kwa jamii yake pamoja na watu wote wa Homa Bay na Wakenya kwa ujumla. Risala zangu za rambirambi si zangu tu bali ni za eneo Bunge la Taveta na watu wake, ambao pia wanamfahamu Senator Otieno Kajwang’. Alipokuwa Waziri wa maswala ya uamiaji, alikuja mpaka kwetu Taveta mara kadhaa ili kutuwezesha kuwa na ofisi iliyofaa pale mpakani. Senator Kajwang’ alikuwa ni mtu wa kupenda utani. Ijapokuwa alikuwa anapenda utani, alikuwa ni mtu aliyechukulia kazi yake kwa bidii sana. Hivyo basi, nataka kuunga mkono wenzangu kwamba Mwenyezi Mungu amweke pahali pema peponi, na pale alipoenda afahamu kuwa ametuacha bado na mapambano ya kimaisha. Yeye ameenda mbele ya haki na ametutangulia ili kututengenezea njia."
}