GET /api/v0.1/hansard/entries/503736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503736,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503736/?format=api",
"text_counter": 131,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "akiwa amefika ulipata kwamba kila mtu alimshangilia na huo mkutano hungeisha kabla hajapewa nafasi ya kuzumgumza maanake wananchi wangelazimisha aongee. Katika wimbo wake wa “bado mapambano”, lazima kuna kitu ambacho alikuwa anahisi kwamba hatujafikia. Kama ni kuhusu ukombozi, alimaanisha hatukuwa tumeupata. Kwa hivyo, wimbo huo, ametuachia sisi ambao ni wachanga kisiasa tuweze kujua kwamba hatujafika na bado tung’ang’ane ili Kenya iweze kuwa mahali pazuri. Kwa hivyo, tunaiombea jamii yake. Tunawaweka katika maombi kwa sababu huu ni wakati mgumu sana na bila nguvu za Mwenyezi Mungu, hawataweza. Sisi sote tuweze kusimama na wao kwa maombi. Ninaamini ya kwamba Mungu ataisimamisha familia yake."
}