GET /api/v0.1/hansard/entries/503774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 503774,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503774/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. ole Ntutu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2535,
        "legal_name": "Patrick Keturet Ole Ntutu",
        "slug": "patrick-keturet-ole-ntutu"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika kwa nafasi hii. Najiunga na wenzangu kutuma rambirambi kwa familia ya ndugu yetu Kajwang’. Kwa niaba ya watu wa eneo Bunge la Narok na Kaunti ya Narok, tunasema poleni sana kwa kumpoteza ndugu yetu Kajwang’. Mimi nilimjua Kajwang’ tulipokuwa tukitengeneza Katiba ya Kenya. Alikuwa anazungumzia sana kuhusu sheria. Wengine wetu ambao wakati huo tulikuwa bado tunafanya kazi katika Serikali, alikuwa anataka tupate Katiba ambayo itawasaidia Wakenya kwa siku zijazo. Nilipokuwa nikifanya kazi Malindi alipokuwa Waziri wa Uhamiaji alikuja Malindi akitaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea huko. Alipoingia mkutanoni, alituuliza ni kwa nini tulikuwa tumekunja nyuso zetu kama watu ambao walikuwa wamekasirika. Kabla ya kucheka, yeye alianza kucheka. Alitufurahisha kwa sababu aliwapenda watu ambao walikuwa wakifanya kazi kwa Serikali. Aliipenda kazi yake na alikuwa anaifahamu vyema. Sisi ambao tumejiunga naye katika Bunge hili, tunamjua kama mtu ambaye akizungumza katika baraza lolote la kisiasa, aliwafurahisha watu. Kwa hayo machache, namwomba Mwenyezi Mungu amuweke marehemu pahali pema peponi."
}