GET /api/v0.1/hansard/entries/503793/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 503793,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/503793/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Asante sana Mheshimiwa Spika. Mimi naungana na viongozi wenzangu siku hii ya leo kwa niaba yangu mwenyewe na familia yangu na kwa niaba ya wananchi wangu wote wa eneo Bunge la Jomvu kutoa rambirambi kwa kifo cha Mheshimiwa Otieno Kajwang’. Leo ni siku ya huzuni sana katika nchi yetu ya Kenya. Nikisema hivyo nachukua yale ambaye niko nayo mimi mwenyewe binafsi juu ya Mheshimiwa Otieno Kajwang’. Miaka mitatu iliyopita nilikuwa kinara wa chama cha ODM katika eneo Bunge la Changamwe. Wakati huo tulifanya kazi pamoja tukishirikiana sote pamoja, na vile vile katika uchaguzi uliopita hivi punde. Yale ambayo yaliweza kutokea kwangu mimi mwenyewe binafsi, katika watu ambao waliniita na kuniambia “pambana, endelea mbele na usife moyo,” mmoja ni Mheshimiwa Otieno Kajwang’. Leo ninasema kuwa hii ni funzo kubwa katika ulimwengu kwa ajili jana mwenzetu kiongozi alikuwa mzima na leo hii tunazungumza akiwa yuko mahali pengine. Kwa hivyo, mimi mwenyewe binafsi na familia yangu na eneo Bunge langu la Jomvu nasema kuwa tunaomboleza pamoja na watu wote na familia zao ili Mungu aweze kumweka mahali pema peponi. Shukrani sana na Mwenyezi Mungu amweke mahali pema."
}