GET /api/v0.1/hansard/entries/504624/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 504624,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/504624/?format=api",
    "text_counter": 418,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kutoa rambi rambi zangu kwa watu wa Kilifi na kwa Wakenya wote kwa ujumla. Ningependa kusema pole kwa Wakenya na familia zote zilizopoteza wapendwa wao. Ningependa kushutumu sana kitendo cha ugaidi na hasa wale waliua kwa sababu mtu hakuitwa Hassan ama Ali. Walioitwa Hassan na Ali waliambiwa wakae pande moja na wengine ambao waliitwa George ama Stephen wakaambiwa wakae upande mwingine. Watu hawa waliambiwa walale wakiangalia chini halafu vichwa vyao vikapasuliwa kwa kupigwa risasi. Hiyo ni aibu kubwa sana na kitendo cha unyama ambacho hakijaonekana katika ulimwengu huu. Wengine wetu tulikuwa tukisoma kwa vitabu na hatukujua kwamba kitendo kama hicho kingefanyika katika Kenya ya leo. Kwa nini nasema hivyo? Hii ni kwa sababu kuna uzembe wa kazi katika Idara ya Polisi hasa katika sekta ya upelelezi. Hata wakipeana habari, hatua haichukuliwi. Tunauliza, nchi hii ina Rais ambaye ana mamlaka? Kama Rais ana mamlaka, kama hawezi kuwaondoa watu hao, anafanya nini katika ofisi yake? Wakenya 40 milioni walimpa uongozi. Lazima achukue fimbo na kuwachapa watu hawa. Hawa ni vijana ambao wana ujuzi katika mambo ya usalama. Tunaona aibu sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}