GET /api/v0.1/hansard/entries/504626/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 504626,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/504626/?format=api",
    "text_counter": 420,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kenya inapoelekea, naona tumekubali watu wapigane kwa sababu ya dini. Haya sio mambo ya dini. Sisi tulizaliwa huko Mombasa. Wengine kama sisi tulizaliwa Mvitheni. Tumekuwa tukilala na ndugu zetu. Watu ambao wamekuwa wakiishi pamoja huko Mombasa wameuwana. Mama anaweza kuwa Mkristo na baba Mwislamu. Ukianza kuwatenga watu wa familia kwa misingi ya baba na mama na kuwaita George, mwingine Ali, leo ukija kumuua mmoja na kumwacha mwingine, tutakuwa tukienda Kenya gani? Serikali ya Jubilee ni lazima ichukue hatua ya kuwafuta kazi watu ambao wamezembea kazini. Hakuna haja ya Rais kuwa Ulaya wakati watu wake wanauwawa. Hatuelewi anafanya nini huko. Kama angekuwa Rais wa nchi nyingine, angekuwa amerudi katika nchi yake kuwatetea watu wake. Asante. Naunga mkono."
}