GET /api/v0.1/hansard/entries/505023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 505023,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505023/?format=api",
    "text_counter": 391,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Asante Mhe. Spika wa Muda. Nishatoa risala zangu za rambirambi kwa jamaa za waliohusika wote. Ni kweli kuwa nchi ya Kenya imekumbwa na maafa. Kenya leo ina matatizo makubwa. Ni nini tunastahili kufanya? Kama Wakenya, tunapaswa kufahamu uzito na upana wa matatizo yanayokumba taifa letu. Je, Kenya inayo sera ya usalama wa ndani wa taifa? Haina. Wajibu wetu ni nini kama Wakenya? Najua kuwa tutalaumiana; eti futa kazi ole Lenku au futa kazi Kimaiyo. Kifungu cha 240 cha Katiba ya nchi kilichobuni baraza la usalama wa taifa kimeanza na Rais, Makamu wa Rais, Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Maswala ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Waziri wa Masuala ya Nje, Inspekta Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Majeshi, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Ujasusi na Mkuu wa Sheria. Hao ni watu watisa. Wakenya tunapaswa kuamua kama tutawafuta watu watisa au tutatafuta suluhisho. Lakini kuwalaumu ole Lenku na Kimaiyo haitakuwa suluhisho ya matatizo yanayoikumba nchi hii. Baraza la Usalama lina watu watisa. Baraza si ole Lenku na Kimaiyo peke yao. Kuna Rais, Makamu wa Rais, Mawaziri watatu, Mkuu wa Majeshi, Inspekta Mkuu wa Polisi, Mkuu wa Sheria na Mkuu wa Masuala ya Ujasusi. Bunge liamue na liseme waende lakini si kuwatisha ole Lenku na Kimaiyo. Hiyo si suluhisho. Leo tumetuma wanajeshi nchini Somalia. Je, mpaka wetu wa Mandera una wanajeshi wanaoulinda? Kwa nini tunashughulika zaidi mle Somalia na mpaka wetu hatuushughulikii? Kwa hivyo, tujiulize matatizo yako wapi. Tutakapopiga parapanda pamoja kuwa ole Lenku afutwe kazi, taasisi itabaki. Ile kamati ya usalama wa taifa bado iko. Hata Kimaiyo akifutwa kazi, yule Kamishna wa Polisi atakayemfuata, atakuwa mmoja wao. Nimesikitika. Wengine wanasema kuwa manaibu wafutwe kazi. Watafutwa vipi ilhali wao sio wanachama wa Baraza la Usalama wa Taifa? Kwa hivyo, tusielekezwe na hamasa na hasira. Tuyajue haya matatizo na tutafute suluhisho mwafaka."
}