GET /api/v0.1/hansard/entries/505076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 505076,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505076/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. ole Sakuda",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 442,
"legal_name": "Moses Somoine ole Sakuda",
"slug": "moses-ole-sakuda"
},
"content": "ovyo ovyo lakini hatujawahi kusikia akiongea mambo ya security ya nchi hii. Tunataka kumwambia Kavuludi akusanye virago vyake na aondoke kwa sababu yeye ndiye anapiganisha watu kule ndani. Tuko na hiyo habari. Serikali ya Jubilee inaendelea kuongea mambo ya maendeleo. Hakuna maendeleo ambayo tunaweza kufanya kama usalama wa wananchi wa Kenya unahatarishwa kila wakati. Mhe. Naibu Spika wa Muda, jana nilikuwa eneo Bunge langu la Kajiado Magharibi. Kulikuwa na maandamano ya akina mama wakisema ya kwamba kwa sababu ya usalama wao, walisha ngamia kule Kajiado Magharibi wataondoka. Ni kwa sababu gani? Wanasema wanaona watu wakiuliwa kwa sababu ya mambo ya misikiti. Hiyo ni kusema namna gani? Nilisimama nikawaambia Kenya hii ni ya Wakenya wote na tuweze kuheshimiana, lakini kwa sababu ya yale matendo ambayo tunayaona, hata usalama Kenya hii unakuwa katika hatari. Ni wakati ambapo tutasimama kama Wabunge na tuseme ya kwamba usalama wa kila Mkenya lazima ulindwe. Kama watu wataenda nyumbani, waende maana kama ni mbaya ni mbaya."
}