GET /api/v0.1/hansard/entries/505098/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 505098,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505098/?format=api",
    "text_counter": 466,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "kitu gani kimefanyika ndio mambo kama hayo yatokee. Tunasikia kuwa wananchi walitolewa kwa basi na wakagawanya kati ya Wakristo na Waislamu. Ni lazima kuyaangalia mambo hayo. Kuongea na kusema ni nani atafutwa kazi au ni nani hatafutwa, ni lazima tuyaangalie kwa sababu si ukweli kuwa watu walipatikana na magaidi ghafla. Gaidi ni nani? Gaidi ni yule mtu ambaye tunakaa naye kwa nyumba. Ni lazima tuangalie hawa magaidi ni akina nani. Sisi wafugaji tunasema kuwa vijana wetu wanaenda kuiba, lakini inajulikana wakienda kupigana. Kwa nini haijulikani hawa magaidi wanatoka wapi na wanaenda wapi? Tungeomba kujua haya mambo yote kwa sababu kwa nini hawa magaidi hawakuwaua watu wote? Viongozi wa upande huo wanafaa kurudi huku ili kuangalia taabu hii inatoka wapi ili ukweli kuhusu ni nini kinachoendelea upatikane. Hatufai kusema ni nani atafutwa kazi au ni nani hatafutwa kazi. Ni lazima viongozi warudi huko ili wajue hii taabu imetokea wapi."
}