GET /api/v0.1/hansard/entries/505110/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 505110,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505110/?format=api",
    "text_counter": 478,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "sababu sisi ni miongoni mwa wale ambao tumeathirika pakubwa katika swala hili. Lakini pengine moja ama mawili ambayo nitazungumzia ni kwamba hivi sasa, nafikiri sote twafahamu ya kwamba hata wale wachezaji katika mpira wakiwa ni wazuri, lakini wanapofanya makosa, lawama zote zinaenda kwa coach . Hali halisi ilivyo katika Kenya yetu kwa maswala ya usalama, imekua ni swala ambalo lazungumzwa kila siku lakini halionekani kupata suluhisho. Ni vyema tukiwa kama viongozi, kama wajumbe, tulitafutie suluhisho jambo hili. Kwa kweli, tulitafutie suluhisho jambo hili. Iwapo tutaliacha kuendelea namna hivi na kulijadili ama kupeana lawama hapa na pale, hatutafika katika zile suluhisho ambazo tuko nazo. Matatizo yapo. Watu wanauawa. Hivi sasa tunavyozungumza, katika Jimbo la Lamu watu hawana ruhusa ya kutoka nje usiku kwa sababu hakuna usalama. Haya yote yamechangia kuzorota kwa uchumi katika sehemu zetu. Kuna umuhimu mkubwa kwa swala hili kuangaziwa pakubwa na sisi viongozi na viongozi wote katika nchi hii. Tukianza kulaumiana hatutapata suluhisho. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha kwamba tumeliangalia swala hili. Watu wote waliopewa majukumu katika maswala haya ni lazima tuangalie kwa sababu hawa ambao wanafariki leo na kesho ni ndugu zetu na tunawajibika kuhakikisha kwamba tumekomesha haya. Hivi sasa watu wanaumia na kuteseka kwa sababu ya tatizo hili la kutokuwa na usalama."
}