GET /api/v0.1/hansard/entries/505112/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 505112,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/505112/?format=api",
    "text_counter": 480,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nataka kutoa risala zangu za rambirambi kwa ndugu zetu wa Mandera, Kapedo na Mombasa kwa sababu ya kuuawa katika njia tatanishi za kupitia hawa AlShabaab . Wakati huu si wakati wa kutoa tu matatizo. Ni wakati wa kuuliza: Ni njia gani mwafaka itatusaidia ili Kenya yetu iwe na usalama? Ingekuwa sawa kwanza tujizatiti katika kulinda mipaka yetu. Lazima kuna ulegevu katika kulinda mipaka yetu. Juzi katika Jimbo la Mombasa, tuliona katika Masjid Musa na Masjid Mina kumepatikana gruneti, bastola na silaha zingine. Silaha hizi zinaingia kutoka wapi na kupitia wapi? Ikiwa walinda usalama wamejua ya kwamba msikiti fulani ama mahali fulani pamekuwa pahali nyeti kwa sababu ya mambo ya Al Shabaab, kwa nini macho yao yote hayawi mahali kama hapo? Kwa nini wale maofisa wetu hawawezi kuweka macho yao katika sehemu kama hizo? Tunashangaa mpaka sasa kusikia Masjid Musa na Masjid Mina kumepatikana silaha. Sisi lazima kwanza tulinde nchi yetu wenyewe katika mipaka yetu kabla hatujaingia Somalia. Jambo la mwisho, Mhe. Naibu Spika wa Muda, wanajeshi wetu wanalipwa duni. Wanapata kidogo cha shilingi 80,000 kwenda kuuza roho zao. Ikiwa wanalipwa pesa ambazo haziwezi kuwapa motisha---"
}